Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 19:22

Sudan Kusini yatishia kuzima vyombo vya habari


Picha ya Maktaba: Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ambaye serikali yake imetishia kuzima vyombo vya habari.
Picha ya Maktaba: Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ambaye serikali yake imetishia kuzima vyombo vya habari.

Serikali ya Sudan Kusini, Jumatatu, imetishia kuvizima vyombo vya habari endapo waandishi wake watafanya mahojiano na waasi.

Shirika la habari la Ufaransa AFP, lilimkariri Waziri wa habari wa serikali ya Sudan Kusini, Michael Makueri, akitoa tamko hilo.

Makueri amesema kwamba watazima vyombo vya habari kama vitafanya mahojiano na muasi yoyote ambaye atazungumzia mipango yake ama sera zake ndani ya Sudan Kusini.

Tahadhari hiyo inakuja baada ya redio moja kufanya mahojiano na kiongozi mmoja wa upinzani.

Sudan Kusini hivi sasa ipo katika mzozo unaozua hali tete katika nchi hiyo changa kuliko zote barani Afrika.

XS
SM
MD
LG