Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 25, 2023 Local time: 16:19

Sudan kusini yatangaza Jonglei yakumbwa na maafa ya kibinadamu.


Naibu katibu mkuu wa Umoja wa mataifa anayeshughulikia masuala ya kibinadamu Valerie Amos katika mkutano na waziri wa masuala ya kijamii wa Sudan Amira al-Fadel Mohamed huko Khartoum.

Baraza la mawaziri Sudan Kusini limetangaza janga hilo katika mkutano maalum ambapo kundi la wapiganaji 6000 la kabila la Lou Nuer lilishambulia baadhi ya miji.

Sudan Kusini imetangaza janga la kibinadamu katika jimbo la Jonglei eneo ambalo limekuwa na mapigano ya mara kwa mara ambayo yameuwa mamia ya watu.

Msemaji wa serikali amesema baraza la mawaziri Sudan Kusini limetangaza janga hilo katika mkutano maalum jana na kuyaomba mashirika ya misaada ya kimataifa kupeleka msaada haraka kwenye jimbo hilo.

Kundi la wapiganaji 6000 kutoka kabila la Lou Nuer lilishambulia miji ya Lukangol na Pibor wiki iliyopita, na kuchoma moto mahema na kusababisha maelfu kukimbia eneo hilo. Pibor ndio eneo wanalotoka watu wa kabila la Murle, ambao wanashutumiwa kwa mashambulizi kwenye eneo la Lou-Nuer mwezi Agosti.

Serikali inasema majeshi yake yameidhibiti Pibor na kusema itajaribu kuandaa mazungumzo ya maridhiano kati ya makabila hayo.

XS
SM
MD
LG