Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 28, 2023 Local time: 22:35

Sudan Kusini yaonya dhidi ya maandamano


Rais wa Sudan kusinI Salva Kiir
Rais wa Sudan kusinI Salva Kiir

Idara ya polisi ya Sudan kusini imepeleka maafisa kwenye mitaa ya mji mkuu wa Juba huku ikionya wananchi dhidi ya kushiriki kwenye maandamano ya kitaifa dhidi ya serikali,yaliyopangwa kufanyika Jumatatu.

Kundi la kiraia kwa jina People’s Coalition for Civil Action limepanga maandamano hayo baada ya kuzindua kampeni ya kuitisha mabadiliko mwezi Julai. Kundi hilo linadai kwamba serikali mpya ya muungano chini ya Rais Salva Kiir haijafanya chochote katika kutatua changamoto zinazowakabili watu wa Sudan Kusini.

Abraham Awlic ambaye ni mmoja ya wanachama wa kundi hilo amesema kwamba tayari wamewafahamisha poslisi kuhusu maandamano hayo kwa njia ya barua ingawa siyo lazima kufanya hivyo. Abraham ameiambia VOA kipindi cha South Sudan in Focus kwamba watu wa Sudan kusini watajitokeza ili kuandamana Jumatatu ikiwa ni haki yao ya kikatiba.

Ameongeza kusema kwamba huwezi kuomba idhini ya kuandamana kutoka kwa serikali inayo kukandamiza. Msemaji wa polisi meja generali Daniel Justin ameonya kwamba maandamano hayo yatavuruga amani, na kamwe hataruhusiwa na serikali.

XS
SM
MD
LG