Mkataba tete wa kusitisha mapigano ulielekea kuendelea Jumanne katika mji mkuu wa Sudan Kusini Juba baada ya siku nne za mapigano yaliyosababisha vifo vya mamia ya watu na maelfu kukimbia makazi yao.
Mazungumzo hayo yaliyoitishwa na rais Salva Kiir na mpinzani wake wa muda mrefu, makamu wa rais Riek Machar yalipokelewa vizuri na wananchi waliochoshwa na mapigano na serikali za nje kutokana na wasiwasi kwamba taifa hilo changa la Afrika linaweza kurudi tena kwenye mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.
Mjini Washington, wizara ya mambo ya nje, ilitoa tahadhari kupitia kwa msemaji wake John Kirby akigusia kuhusu mapigano ya holela katika sehemu za Juba licha ya kuwepo na utululivu.
Balozi huyo amesema hafikirii kama Marekani itamrudisha balozi wake kutoka huko licha ya kile alichokiita amri ya kuondoka kwa wafanyakazi wake wasio wa dharura kuondoka ubalozini hapo.