Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 04:30

Kituo cha Eye radio chafungwa Sudan Kusini


Mwakilishi maalum wa Marekani Sudan Kusini Bw.Donald Booth akizungumza na waandishi wa habari.
Mwakilishi maalum wa Marekani Sudan Kusini Bw.Donald Booth akizungumza na waandishi wa habari.

Kituo kimoja maarufu cha radio nchini Sudan Kusini ambacho kimeanzishwa kwa msaada wa Marekani kimefungwa Ijumaa na maafisa usalama, mwandishi mmoja wa habari ameeleza.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters mwandishi wa habari mwandamizi, Nichola Mandil wa kituo cha Eye radio mjini Juba , maafisa usalama walifika na kusimamisha matangazo yao bila ya kutoa sababu zozote.

Kituo cha Eye radio kimefungwa rasmi na idara ya taifa ya usalama amesema na kuongezea kuwa maafisa watatu wa usalama wamefunga studio tatu za kituo hicho na kuondoka na funguo. Wameamuru waandishi wote kuondoka kwenye kituo hicho haraka na hivi sasa tuko katika utaratibu wa kwenda nyumbani amesema Mandil na kuongezea kwamba mkuu wa kituo hicho atakutana baadaye na mkurugenzi mkuu wa usalama wa taifa kupata maelezo zaidi.

XS
SM
MD
LG