Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 10:34

Marekani, Umoja wa Mataifa waonya kuhusu ongezeko la ghasia Sudan Kusini


Moshi mweusi umetanda mjini Juba, Sudan Kusini wakati wa ghasia za mwezi Julai.
Moshi mweusi umetanda mjini Juba, Sudan Kusini wakati wa ghasia za mwezi Julai.

Wawakilishi wa Marekani na Umoja wa Mataifa wameonya katika mikutano tofauti hapo jana juu ya kusambaa kwa mivutano na uwezekano wa ghasia nchini Sudan Kusini.

Mwakilishi wa Marekani katika baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu huko Geneva, Keith Harper amesema wana habari za uhakika kwamba serikali ya Sudan Kusini hivi sasa inawalenga raia katika jimbo la Central Equatorial na kujitayarisha kwa mashambulizi makubwa katika siku au wiki zijazo.

Dai hilo haraka lilikanushwa na mwenzake wa Sudan Kusini, na balozi wa Sudan Kusini, Kuol Alor Kuol Arop kwamba kuna mipango yoyote ya majeshi ya kufanya mashambulizi, aliyasema hayo katika mahojiano na shirika la habari la Associated Press.

Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Samantha Power ameiambia VOA huko New York kwamba tunaelezea wasi wasi wetu, tunaitaka serikali ya Sudan Kusini kutosonga mbele na mashambulizi ambayo wameyapanga.

Jana Jumatano huko mjini Juba, watalaamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameonya viwango visivyoelezeka vya ghasia na mivutano ya kikabila kote katika taifa hilo lilikumbwa na vita.

Yasmin Sooka wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini ambayo inafuatilia hali amesema wanatarajiwa mapigano kuongezeka katika kipindi hiki wakati msimu wa kiangazi unaingia.

Kundi la wafuatiliaji wa kimataifa waliizuiwa na serikali kwenda Central Equatorial kwenda kuchunguza ukiukaji wa makubaliano ya amani ya nchi hiyo mapema wiki hii.

XS
SM
MD
LG