Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 13:02

Sudan Kusini kutosimamisha uhusiano na Sudan


Serekali ya Sudan Kusini hapo Jumatano imesema licha ya kiongozi wa zamani wa uasi Riek Machar kutibiwa katika hospitali ya mjini Khartoum, Sudan kwa matatizo ya kifua na majeraha ya mguuni, hali hiyo haito athiri uhusiano baina ya nchi hizo mbili.

Mawien Makol Ariik, ambaye ni msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Sudan Kusini amesema Juba itaendelea kufanya kazi na Khartom katika biashara na masuala maengine ya ushirikiano.

Licha ya kwamba uwepo wa Machar mjini Khartoum unaendana na ziara ya wiki hii ya ujumbe wa Sudan Kusini unaoongozwa na makamu wa kwaza wa rais Taban Deng Gai, ambaye anawakilisha upinzani wa SPLM katika upinzani, Ariik amesema Juba inahakikisha kuwa inaendeleza uhusiano mzuri na Khartoum.

XS
SM
MD
LG