Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 22:26

Khartoum yasema itaishambulia Sudan Kusini


Baadhi ya wanajeshi wa Sudan wakiwa katika lindo
Baadhi ya wanajeshi wa Sudan wakiwa katika lindo

Rais wa Sudan asema hatosita kuishambulia Sudan kusini katika mzozo wa mji wa mpakani.

Rais wa Sudan, Omar Al–Bashir ameapa kuivunja serikali ya Sudan Kusini.Bwana Bashir alisema hayo katika hotuba Jumatano katika mkutano kwenye mji mkuu Khartoum akitishia kuipindua serikali ya Sudan Kusini na kukiondoa chama chake tawala cha SPLM.

Bwana Bashir alisema jeshi lake liko tayari kuchukua tena udhibiti wa mji wa Heglig ulio mpakani ambao unazalisha takriban nusu ya mafuta ya Sudan.

Sudan inataka majeshi ya Kusini yaondoke katika mji huo wakati Kusini imeshutumu Sudan kwa kufanya mfululizo wa mashambulizi kadhaa. Nchi hizi mbili zimeshindwa kutatua mzozo wa mipaka, mafuta na uraia uliozuka wakati wa uhuru wa Kusini Julai mwaka jana.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilisema wiki hii litafanya kila juhudi kuhakikisha pande hizo mbili zinamaliza mzozo na kurejea katika maridhiano.

XS
SM
MD
LG