Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 05, 2023 Local time: 18:31

Sudan Kusini kuruhusu misaada kupelekewa waathiriwa


Rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar wakibadilishana hati ya mkataba wa amani, Addis Ababa, Ethiopia Mei 9, 2014
Rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar wakibadilishana hati ya mkataba wa amani, Addis Ababa, Ethiopia Mei 9, 2014

Rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar walikutana ana kwa ana kwa mara ya kwanza Ijumaa tangu kuzuka kwa ghasia yapata miezi mitano iliyopita na kutia saini makubaliano hayo mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa huko Sudan Kusini ametoa mwito wa kupelekwa mara moja kwa msaada ja wa dharura kufuatia kutiwa saini makubaliano ya kusitisha mapigano ya kikabila ambayo yamedumu kwa miezi kadhaa.

Toby Lanzer, alipeleka ujumbe huo kupitia mtandao wa Twitter Jumamosi,akisema barabara nchini humo zinahitaji kufunguliwa ili malori ya misaada yaweze kupita na kuwapelekea watu msaada wa dharura unaohitajika sasa.

Rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar walikutana ana kwa ana kwa mara ya kwanza Ijumaa tangu kuzuka kwa ghasia yapata miezi mitano iliyopita na kushiriki katika maombi ya pamoja mjini Addis Ababa, Ethiopia kabla ya kutia saini makubaliano hayo.

Wote wawili waliahidi kusitisha uhasama wote baina yao na kufungua njia ili misaada ya kibinadamu iweze kuwafikia waathiriwa.

Walikubaliana pia kuwa njia bora zaidi ni kuwa na serikali ya mpito inayotoa fursa kwa nchi yao kusonga mbele. Lakini hapakutolewa maelezo juu ya nani atakayekuwa sehemu ya utawala huo wa muda.
XS
SM
MD
LG