Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 28, 2025 Local time: 02:24

Sudan Kusini inawasaka wabadilishaji fedha haramu


Raia wa Sudan Kusini akishikilia fedha inayotumika nchini humo.
Raia wa Sudan Kusini akishikilia fedha inayotumika nchini humo.

Serikali ya Sudan Kusini inawasaka wabadilishaji fedha haramu ili kujaribu kuzuia sarafu ya Sudan Kusini paundi kushuka zaidi dhidi ya dola ya kimarekani.

Kikosi mchanganyiko cha maafisa polisi, jeshi na idara ya usalama wa taifa walionekana wakizunguka kwenye masoko kadhaa ya ubadilishaji fedha mjini Juba katika wiki iliyopita. Mfanya biashara mmoja wa ubadilishaji fedha ambae aliomba jina lake lisitajwe kwa ajili ya usalama alisema msako huo utamzuia kujipatia chanzo pekee anachotegemea cha mapato yake. Mfanyabiashara huyo wa soko haramu la fedha alisema hana maisha mengine zaidi ya kazi hiyo anayoifanya.

Wiki iliyopita benki kuu ya Sudan Kusini ilisema itaingiza dola zaidi ya Marekani kwenye uchumi nchini humo ili kuzuia mdororo zaidi wa paundi ya Sudan Kusini. Dola ya kimarekani hivi sasa inabadilishwa kwa paundi 250 za Sudan Kusini ikiwa imeongezeka kutoka paundi za Sudan Kusini 215 wiki moja iliyopita kwenye soko haramu la fedha.

XS
SM
MD
LG