Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 23:35

Sudan Kaskazini yataka baraza la pamoja la utawala na kusini


Abyei inavyonekana katika picha
Abyei inavyonekana katika picha

Serikali ya Khartoum inapendekeza kuteuliwa mwenyetiki wa baraza hilo kwa zamu kati ya kaskazini na kusini

Serikali ya Sudan kaskazini imependekeza kutatua mzozo wake na serikali ya kusini kwa kuteuwa baraza la pamoja la utawala kwa ajili ya jimbo lenye utajiri wa mafuta la Abyei.

Serikali ya Khartoum inapendekeza kuteuliwa mwenyetiki wa baraza hilo kwa zamu kati ya kazkazini na kusini. Na inaeleza kwamba mto wa Bahar al-Araba unabidi kuwa mpaka unaowatengenisha vikosi vya kaskazini na kusini.

Vikosi vya Sudan kaskazini vilichukua udhibiti wa Abyei mwezi Mei 21 na kusababisha maelfu ya watu kukimbia eneo hilo na kuzusha hofu kwamba kaskazini na kusini zinaweza kurejea tena katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Serikali ya Khartoum inatowa wito wa kuwepo kikosi cha amani cha Afrika huko Abyei badala ya walinda amani wa kimataifa.

Sudan kusini inatarajiwa kutangaza uhuru wake Julai tisa, baada ya wananchi wa huko kuamua kujitenga na kaskazini wakati wa kura ya maoni ya mwezi Februari. Abyei ilitarajiwa kupiga kura siku hiyo hiyo mwezi January kama ijiunge na kaskazini au kusini lakini pande zote hazikukubalina nani aliye na uhalali wa kupiga kura.

Serikali ya kaskazini imepinga wito kutoka Marekani, Umoja wa Mataifa na Sudan Kusini kuondowa wanajeshi wake kutoka Abyei. Hata hivyo pande hizo mbili zilikubaliana siku ya Jumatatu kuunda eneo la usalama lisilokuwa na shughuli za kijeshi kati ya Kaskazini na Kusini.

XS
SM
MD
LG