Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 09, 2023 Local time: 11:22

Sudan kaskazini yaendelea kudhibiti Abyei


walinda amani wa umoja wa mataifa wakifanya doria katika mji wa Abyei
walinda amani wa umoja wa mataifa wakifanya doria katika mji wa Abyei

Ujumbe wa umoja wa mataifa nchini Sudan umeripoti kutokea uchomaji moto na wizi katika mji wa Abyei

Ujumbe wa umoja wa mataifa nchini Sudan umeripoti kutokea uchomaji moto na wizi katika mji wa Abyei unaogombaniwa ambao Sudan kaskazini ulichukua udhibiti wake siku mbili zilizopita.

Katika taarifa yake ujumbe huo umelaani vikali ghasia zinazoendelea jumatatu na umesema jeshi la kaskazini linawajibika kushikilia sheria katika eneo linalodhibiti.

Umoja wa mataifa inalaumu uchomaji moto na wizi unaofanywa kwa kutumia silaha. Lakini taarifa ya UN haikufafanua zaidi.

Mapema jumatatu wajumbe wa baraza la usalama la umoja wa mataifa walitaka Sudan kaskazini kuondoa majeshi yake huko Abyei .

Sudan kusini inasema upande wa kaskazini kuchukua udhibiti wa eneo hilo ni kinyume cha sheria na imeomba msaada kutoka jumuiya za kimataifa.

Sudan kaskazini na kusini zilipigana vikali kugombea eneo hilo lenye utajiri wa mafuta katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka 21 na kumalizika mwaka 2005.

XS
SM
MD
LG