Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 27, 2024 Local time: 02:28

Sudan Kaskazini kuondoa raia wa kusini jeshini.


Raia wa Darfur waliopoteza makazi yao.
Raia wa Darfur waliopoteza makazi yao.

Wanajeshi raia wa Sudan Kusini wanaondolewa kwenye jeshi la kaskazini kwa hafla maalum.

Jeshi la Sudan kaskazini linawaondoa jeshini mwake wanajeshi wapatao 15,000 raia wa kusini wakati kusini wakijiandaa kutangaza uhuru wao.

Kituo habari cha Sudan kinachounga mkono serikali kinaripoti kutakuwa na sherehe za kuwaondoa wanajeshi hao huko Khartoum alhamisi.

Jamhuri mpya ya Sudan Kusini inategemewa kutangaza uhuru wake Jumamosi. Kusini na kaskazini wanajaribu kutenganisha shughuli zao lakini pande hizo mbili bado hazijasuluhisha masuala ya mipaka na faida ya mafuta.

Jeshi la kaskazini kwa sasa bado linapigana na makundi ya kusini katika jimbo linaloshikiliwa na kaskazini la Kordofan Kusini.

Wakati huo huo matayarisho yanaendelea kwa sherehe za Jumamosi katika mji mkuu wa kusini Juba . Maafisa wamefunga mitaa ili waandaaaji waweze kujiandaa kwa sherehe kuu na shughuli nyingine.

XS
SM
MD
LG