Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 02:27

Algeria: Jeshi latangaza vita dhidi ya ufisadi serikalini


Rais wa muda wa Algeria Abdelkader Bensalah.
Rais wa muda wa Algeria Abdelkader Bensalah.

Baadhi ya maafisa waandamizi serikalini, ikiwa ni pamoja na waziri wa fedha, aliyekuwa waziri mkuu, na matajiri wenye ushawishi mkubwa wa kisiasa, wamekuwa wakifanyiwa uchunguzi tangu aliyekuwa rais wa muda mrefu wa nchi hiyo, Abdelaziz Bouteflika, kulazimishwa kujiuzulu tarehe mbili mwezi Aprili.

Shirika la habari la Reuters limeripoti kwamba mkuu wa jeshi Luteni Jenerali Ahmed Gaed Salah hakutoa majina ya washukiwa hao, lakini akaahidi kuisaidia idara ya mahakama katika mchakato wa kuwafungulia mashtaka ili ufanyike kwa njia ya uwazi bila uingiliaji kati kutoka nje.

Katika hotuba aliyoitoa kwenye kambi ya kijeshi kwenye mji wa Mashariki wa Constatine, Luteni Jenerali Salah alisema kuwa nchi hiyo itatokomeza ufisadi na wahusika kuchukuliwa hatua zifaazo, za kisheria.

"Idara ya mahakama iko huru kutoka shinikizo zote na nchi hii itatakaswa kutoka kwa ufisadi," alisema.

Mkuu huyo wa jeshi alizungumza saa chache tu baada ya aliyekuwa waziri mkuu Ahmed Ouyahia, kufikishwa mahakamani.

Ouyahia alifutwa kazi siku mbili kabla ya Rais Bouteflika kujiuzulu, katika mabadiliko kwenye baraza la mawaziri.

Matajiri wasiopungua watano, baadhi yao wakiwa ni wandani wa Bouteflika, wamekamatwa kwa tuhuma za ufisadi, huku nchi hiyo ikijitayarisha kwa uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika tarehe nne mwezi Julai.

XS
SM
MD
LG