Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 23:18

Majeshi ya Sudan yashutumiana kufanya mashambulizi


Majeshi ya Sudan yashutumiana kufanya mashambulizi
Majeshi ya Sudan yashutumiana kufanya mashambulizi

Jeshi la Sudan linayashutumu majeshi hasimu ya kusini kwa kuyashambulia majeshi ya Sudan yaliyo kuwa kwenye mlolongo wa msafara wa majeshi ya Umoja wa Mataifa katika eneo lenye utajiri wa mafuta la Abyei. Maafisa wa serikali ya Kusini wanakanusha shutuma hizo.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wanasema watu wawili walijeruhiwa katika tukio hilo lililotokea katika mji wa Dokura, ambalo wamelilaani kuwa ni shambulizi la uhalifu. Jeshi la Sudan lilisema lilipata hasara kubwa lakini halikufafanua zaidi.

Majeshi kutoka kaskazini na kusini yalikubaliana kufanya doria zote za pamoja katika eneo la Abyei. Serikali za kaskazini na kusini zinajaribu kutatua masuala muhimu kabla ya kusini kuwa taifa huru hapo Julai 9, ikiwa ni pamoja na hali ya baadae ya Abyei.

Kura ya maoni kama Abyei iungane na kaskazini au kusini ilipangwa kufanyika mwezi Januari, lakini haikufanyika kwa sababu pande hizo mbili hazikukubaliana juu ya nani alikuwa na haki ya kupiga kura.

XS
SM
MD
LG