Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 12:10

China yazitaka nchi za Sudan kutatua tofauti zao


Bidhaa zikiwasili katika bandari ya Kosti jimbo la White Nile, Sudan Kusini
Bidhaa zikiwasili katika bandari ya Kosti jimbo la White Nile, Sudan Kusini

Serikali ya China inasihi nchi za Sudan kutatua tofauti zao ili kufungua njia bora ya uuzaji wake wa mafuta nje ya nchi

China inazitaka Sudan na Sudan Kusini kutatua mgogoro wao ambao unazuia mtiririko wa uuzaji mafuta nje ya nchi kutoka Kusini.

Beijing inanunua takribani asilimia tano ya mafuta yake yote inayouza nje ya nchi kutoka Sudan Kusini.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Jumanne alisihi pande hizo mbili za Sudan kufanya “stara” na kutumia njia mbadala ili kutatua tofauti zao.

Sudan Kusini ambayo haipakani na bahari yeyote inategemea mabomba ya jirani zake wa kaskazini na bandari ya bahari ya Sham kusafirisha nje ya nchi mafuta yake.

Sudan ilisema ilisitisha uuzaji mafuta wa Sudan Kusini nje ya nchi kwa sababu taifa hilo jipya la Kusini linadaiwa dola milioni 730, ada ya usafirishaji.

Sudan Kusini inasema Khartoum inaitoza ada kubwa ya usafiri na mapato na kupelekea vita vya kiuchumi.

Sudan Kusini ilichukua udhibiti wa kiasi cha asilimia 75 cha mafuta ya Sudan, wakati ilipokuwa taifa huru Julai 9.

Nchi hizo mbili bado zinafanya mazungumzo juu ya namna ya kushirikiana mapato ya mafuta. Pia hawajasuluhisha suala la upande gani utadhibiti eneo la Abyei lenye utajiri wa mafuta.

XS
SM
MD
LG