Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 27, 2024 Local time: 03:17

Wanawake na watoto wakimbia Abyei


Msichana wa Sudan Kusini akishikilia bendera ya eneo hilo.
Msichana wa Sudan Kusini akishikilia bendera ya eneo hilo.

Mamia ya wanawake na watoto wanalikimbia eneo lenye mzozo la Abyei nchini Sudan,ambako mapigano ya wiki hii yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 70.

Mashahidi wanasema mapambano yalihusisha wapiganaji wa Misseriya ambao wanaushirika na Sudan kaskazini na wanaume wa kabila la Ngok Dinka ambao wanaiunga mkono Kusini. Wote maafisa wa Kusini na kaskazini walishutumiana kuwa majeshi ya pande zote yanaunga mkono ghasia. Majeshi yote yalikana kuhusika kwa njia yeyote.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, P.J. Crowley, alilaani mapigano hayo ya Alhamisi na kuzisihi pande zote kuepuka kuchokozana na hivyo kusababisha mapigano zaidi.

Ghasia zimesambaa huko Abyei wakati Sudan Kusini ikijitayarisha kujitenga kutoka kaskazini mwezi July.

Sudan Kusini kwa kura nyingi iliamua kujitenga kutoka kaskazini mwezi January wakati wa kura ya maoni ambapo viongozi wa kaskazini wamesema wanakubali maamuzi hayo.Hata hivyo pande zote bado hazijakubaliana kuhusu hali ya baadae ya mkoa wenye utajiri wa mafuta wa Abyei ambapo unapakana kati ya Kusini na Kaskazini.


XS
SM
MD
LG