Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 12, 2024 Local time: 22:50

Sudan na Sudan Kusini zafikia makubaliano


Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir alipokutana na Rais wa Sudan Omar Al Bashir huko Juba.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir alipokutana na Rais wa Sudan Omar Al Bashir huko Juba.

Rais Omar Al Bashir kwenda Sudan Kusini kutia saini makubliano ya mipaka na uraia.

Sudan na jirani yake Sudan Kusini zimeleza kwamba zimefikia makubaliano ya awali juu ya maswala matatu makuu yaliyosalia baada ya nchi hizo kutengana rasmi mwaka jana. Mwandishi wa VOA mjini Addis Ababa Peter Heinlein anaripoti kuwa rais wa Sudan Omar al-Bashir anatazamiwa kwenda Juba mji mkuu wa Sudan Kusini kwa sherehe rasmi za kutia saini makubaliano hayo. Mazungumzo hayo yaliyoanza kwa mabishano makali mapema mwezi huu yalikamilika huku pande zote mbili zikionyesha nia mpya ya maelewano. Wajumbe kutoka Khartoum na Juba walikaa pamoja na kuzindua mikataba inayozilazimu nchi zote mbili kushirikiana na kutanzua maswala makuu baina yao kama lile la mpaka na uraia. Swala lenye ugumu zaidi la mafuta liliwekwa pembeni hadi pale makubaliano juu ya uraia na mpaka yatatatiwa saini na marais wote wawili. Hii itakuwa ziara kwa kwanza ya rais Bashir Sudan Kusini tangu alipohudhuria sherehe rasmi za taifa hilo mwezi Julai mwaka jana. Lakini hakuna tarehe iliyotangazwa kusaini makubaliano hayo ingawa maafisa wanasema huenda ikawa katika muda wa wiki chache. Mwakilishi wa Umoja wa Afrika katika mazungumzo hayo ambaye pia ni rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki alisema makubaliano juu ya maswala hayo mawili yalifikiwa baada ya pande zote mbili kuacha kutupia lawama kali zilizoshuhudiwa katika mikutano ya hapo awali.

XS
SM
MD
LG