Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 14:31

Suda Kusini yapeleka kikosi cha kulinda amani DRC


Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir akiwa katiga ghafla ya kwaanga wanajeshi wa jeshi la watu wa Sudan Kusini, mjini Juba, wakielekea DRC kulinda amani Desemba 28, 2022.
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir akiwa katiga ghafla ya kwaanga wanajeshi wa jeshi la watu wa Sudan Kusini, mjini Juba, wakielekea DRC kulinda amani Desemba 28, 2022.

Sudan Kusini inatuma wanajeshi 750 kujiunga na Kikosi cha Afrika Mashariki kinachojaribu kuleta amani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, licha ya yenyewe kukabiliwa na kurejesha amani nyumbani.

Rais Klva Kiir, alituma rasmi wanajeshi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kujiunga na kikosi cha kanda ya Afrika Mashariki kinacholenga kumaliza miongo kadhaa ya umwagaji damu nchini humo.

Wanajeshi hao wanaungana na vikosi kutoka Kenya, Burundi na Uganda, katika kile kinachojulikana kama mtihani kwa uwezo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kujibu ghasia katika eneo hilo na kuleta utulivu nchini.

Akihutubia wanajeshi mjini Juba kabla ya kuondoka, Rais Kiir alishauri kikosi hicho kudumisha weledi wa hali ya juu.

"Mnakwenda na dhamira ya kufanikiwa kuleta amani Kongo. Sasa mnakwenda kwenye jukumu la kulinda amani, kofia zenu pekee ndizo zitabadilika na kuwa za bluu, kwa sababu mtashiriki katika operesheni ya pamoja ya nchi zote za Afrika Mashariki. Nawasihi mkaonyeshe nidhamu na kufuata amri pamoja na kutekeleza maagizo."

Pia aliwaagiza wanajeshi kutofanya uhalifu kama vile ubakaji.

“SPLA wakati wa mapambano ya ukombozi ilikuwa na nidhamu kubwa. Sitaki muende kusababisha vurugu au uhalifu. Msiende kufanya ubakaji wa wanawake na wasichana."

Waziri wa Ulinzi na Masuala ya wanajeshi wa zamani Angelina Teny, alisema kwamba kama mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Sudan Kusini ina mchango katika usalama na utulivu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Alisema, “Tuliombwa kuchangia kikosi, na tumekuwa tukijiandaa kwa muda wote huu na kikosi kiko tayari. Wamepokea tu maagizo yao ya mwisho kutoka kwa rais na amiri jeshi mkuu, sasa watakuwa njiani kwa ajili ya operesheni hiyo.

Angelina Tenny alisema Jumuiya ya Afrika Mashariki imetoa uungaji mkono wa kikanda kwa kupelekwa kwa wanajeshi wa Sudan Kusini mashariki mwa DRC.

Alielezea kupelekwa kwa wanajeshi wa nchi hiyo ni hatua nzuri inayofaywa na nchi inayopambana na maswala yake ya usalama.

Wanajeshi wa Sudan Kusini watawekwa katika mji wa Goma, ambako watafanya operesheni ya kurejesha hali ya kawaida katika eneo hilo, ambako wanajeshi wa Kongo wanapambana na kundi la waasi la M23, ambalo linashutumiwa kuwalenga raia katika mzozo uliodumu kwa takriban muongo mmoja.

XS
SM
MD
LG