Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 08, 2024 Local time: 15:03

Subianto amekutana na XI


Rais wa Indonesia Prabowo Subianto
Rais wa Indonesia Prabowo Subianto

Rais wa Indonesia Prabowo Subianto ameahidi kuendeleza uhusiano wa karibu na China, wakati wa kikao na rais wa China Xi Jinping mjini Beijing, leo Jumamosi.

Hii ni mara kwanza kwa Subianto kusafiri nje ya nchi tangu alipoingia ofisini wiki tatu zilizopita.

Subianto anatafuta namna ya kuimarisha uhusiano kati ya Indonesia na China ambayo ni mshirika mkubwa wa Indonesia kibiashara na muhimu kwa wawekezaji.

Hii ni mara ya pili ameitembelea Beijing mwaka huu, mara ya kwanza ilikuwa mwezi April akiwa rais mteule ambapo pia ilikuwa safari yake ya kwanza nje ya nchi baada ya kushinda uchaguzi wa urais mwezi Februari.

Xi ameahidi kuusaidia utawala wa Subianto, na kumshukuru kwa kuchagua kutembelea China kwanza, akiongezea kwamba anaamini Indonesia itachukua hatua za maendeleo, na kunakili mafanikio ya kitaifa.

Forum

XS
SM
MD
LG