Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 16:19

Strauss-Kahn apunguziwa masharti ya dhamana


Mkuu wa zamani wa IMF Dominique Strauss-Kahn (L) na mkewe Anne Sinclair wakiingia mahakamani
Mkuu wa zamani wa IMF Dominique Strauss-Kahn (L) na mkewe Anne Sinclair wakiingia mahakamani

Ataruhusiwa kuwa huru lakini hakurudishiwa pasi yake ya usafiri na waendesha mashitaka wanasema kesi haijafutwa

Jaji mmoja wa New York amemwachia huru mkuu wa zamani wa shirika la IMF, Dominique Strauss-Kahn kwa dhamana yake mwenyewe Ijumaa, kufuatia mashaka makubwa katika uaminikaji wa mwanamke aliyedai kubakwa na Strauss-Kahn.

Kesi hiyo imebadilika vikubwa lakini waendesha mashitaka wanasema "hatujafuta kesi yenyewe."

Kuachiliwa kwa Strauss-Kahn kunampunguzia masharti makali aliyowekewa awali, ikiwa ni dhamana ya dolla millioni sita, na kuwekwa katika kizuizi cha nyumbani katika mtaa mmoja wa kitajiri mjini New York.

Waendesha mashitaka wanatilia mashaka maelezo mengi ya mlalamikaji licha ya kuwa vipimo vya DNA vilionyesha dalili za kitendo cha ngono. Waendesha mashitaka walieleza mashaka yao kwa timu ya utetezi ya Strauss-Kahn ikiwa ni pamoja na kwamba mlalamikaji huyo "hakusema ukweli mtupu katika ombi lake la uhamiaji hapa Marekani kutoka nchi yake ya Guinea."

XS
SM
MD
LG