Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 21:30

Marekani yalaani ghasia za uchaguzi Uganda


Uchaguzi Uganda
Uchaguzi Uganda

Marekani imelaani vitendo vya ghasia vilivyotokea Jumatatu katika kampeni za uchaguzi mjini Kampala, Uganda, ambapo mtu mmoja aliuawa.

Mark Toner kwa kiingereza
please wait

No media source currently available

0:00 0:00:53 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Mark Toner alisema katika maelezo kwa waandishi wa habari leo kwamba Marekani imeingiwa na wasiwasi kutokana na kushikiliwa kwa mgombea urais Kizza Besigye na wafuasi wake kufyatuliwa mabomu ya machozi.

Alisema "masharti namna hiyo katika ukusanyikaji wa umma, hasa yanapofanyika kwa upande mmoja tu katika uchaguzi, yanaongeza mvutano katika mazingira ambayo tayari yana mvutano."

Msemaji Toner alisema Marekani inatoa rambirambi zake kwa ndugu na marafiki wa mtu aliyeuawa, na kusema kwamba Marekani inatumaini vitendo kama hivyo havitarudiwa tena.

XS
SM
MD
LG