Spika wa Baraza la Wawakilsihi Nancy Pelosi amewasili Jumatatu nchini Singapore kwa ziara ya siku mbili, akiongoza ujumbe wa bunge la Marekani huko Asia huku kukiwa na uvumi kwamba safari hiyo inaweza kujumuisha kupitia nchini Taiwan.
Wizara ya mambo ya nje ya Singapore ilisema Pelosi atakutana na Waziri Mkuu Lee Hsien Loong na maafisa wengine.
Katika taarifa Jumapili, Pelosi alisema anaongoza kundi la wabunge wengine watano wa Chama cha Demokrat huko Asia kuthibitisha ushirikiano wa nguvu na usiotetereka wa Marekani kwa washirika wetu na marafiki katika eneo hilo.
Hakutaja kama atakaidi China kwa kupitia Taiwan katika safari ambayo inajumuisha Malaysia, Korea Kusini na Japan kati ya ziara zilizopangwa za ujumbe wa Marekani.