Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 15:04

Mzozo kati ya Iraq na Uturuki waongezeka


Mzozo wa kidiplomasia unazidi kuwa mkali kufuatia kupelekwa kwa wanajeshi wa Uturuki na vifaru huko nchini Iraq, huku Waziri Mkuu wa Iraq akiishutumu Ankara kwa kile alichookitaja kama kutozingatia maazimio ya kuondoa majeshi na kutisha kutumia nguvu za kijeshi.
Mzozo wa kidiplomasia unazidi kuwa mkali kufuatia kupelekwa kwa wanajeshi wa Uturuki na vifaru huko nchini Iraq, huku Waziri Mkuu wa Iraq akiishutumu Ankara kwa kile alichookitaja kama kutozingatia maazimio ya kuondoa majeshi na kutisha kutumia nguvu za kijeshi.

Mzozo wa kidiplomasia unazidi kukithiri kufuatia kupelekwa kwa wanajeshi wa Uturuki na vifaru huko nchini Iraq, huku Waziri Mkuu wa Iraq akiishutumu Ankara kwa kile alichookitaja kama kutozingatia maazimio ya kuondoa majeshi na kutisha kutumia nguvu za kijeshi.

Mzozo wa kidiplomasia unazidi kuwa mkali kufuatia kupelekwa kwa wanajeshi wa Uturuki na vifaru huko nchini Iraq, huku Waziri Mkuu wa Iraq akiishutumu Ankara kwa kile alichookitaja kama kutozingatia maazimio ya kuondoa majeshi na kutisha kutumia nguvu za kijeshi. Kwa upande wake Uturuki imepuuza onyo hizo licha ya shinikizo za kimataifa kutoka kwa nchi ambazo zinasema kwamba kuwepo kwa wanajeshi hao ni muhimu kwani wanalinda vikosi vinavyopigana na magaidi wa Islamic State.

Akitoa onyo hiyo kwa serikali ya Uturuki, waziri wa mambo ya nje wa Iraq, Ibrahin Al Jaafar, alisema "iwapoo itabidi Iraq kupigania uhuru wake, basi tutafanya hivyo."

Vitisho hivyo vimekuja wakati ambapo Baghdad inaishutumu Ankara kwa kuondoa wanajeshi wachache tu ambao walikuwa wanalinda kampi za mazoezi mjini Bashiqa, eneo la Kaskazini mwa Iraq. Lakini Waziri mkuu a Uturuki Aahmet Davutoglu amevipuuza vitisho hivyo na kusema kwambayafaa Iraq ijishugulishe na kupambana na kundi la Islamic State.

Sinan Ulgen, ambaye ni msomi wa taasisi ya Carnegie nchini Ubelgiji, anasema licha ya vitisho hivyo, Ankara haina nia ya kubadilisha msimamo wake.

Anasema:“Waziri mkuu Davutoglu amesema Uturuki itaendelea kuhifadhi wanajeshi wake kuambatana na makubaliano na mamlaka za kikurdi katika eneo hilo. Kusema kwamba Baghdad inaweza kutoa maamuzi kuhusu uwepo wa majeshi ni kama kumaanisha kwamba Iraq inadhibiti eneo hilo. Kama tujuavyo, maeneo makubwa ya Iraq hayadhibitiwi na Baghdad.”

Ankara inaendelea kishirikiana na serikali ya maeneo kikurdi, hali ambayo imesababisha kutoelewana na Baghdad. Vikosi vya kikurdi vya Iraq sasa vinadhibiti sehemu kubwa ya Kaskazini mwa Iraq.

Aydin Selchen, ambaye anasimamia afisi za kibalozi katika eneo la kikurd huko Iraq, anasema Ankara inaamini kwamba Baghdad ndiyo itakuwa ya kwanza kubadilisha msimamo wake.

“Kwanza kabisa, haitakuwa na faida yoyote kusukuma nje ya Bashika mmoja wa washirika wa NATO na ambaye ni jirani mwema. Pili, hawana uwezo wa kufanya hivyo,” amesema Selchen.

Serikali ya Mareka imeitaka Amnkara kuyaondoa majeshi yake, msimamo ambao unaungwa mkono na muungano wa mataifa ya Kiarabu yaani Arab League.

XS
SM
MD
LG