Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 19, 2025 Local time: 17:50

Sudan Kusini yatangaza kuondoa majeshi Heglich


Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (L) akiwa na Rais wa Sudan Omar al-Bashir
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (L) akiwa na Rais wa Sudan Omar al-Bashir

Wiki hii Rais Bashir alitishia kuingia katika vita na Suda Kusini na kuifundisha somo serikali ya nchi hiyo

Sudan Kusini inasema inaondoa majeshi yake kutoka machimbo ya mafuta ya Heglig ambayo yalitekwa kutoka Sudan siku 10 zilizopita na kuchochea wasi wasi wa kuzuka vita.

Msemaji wa serikali aliwaambia waandishi wa habari Ijumaa kwamba Rais Salva Kiir ameagiza kuondolewa majeshi kutoka Heglich, ambayo pia inajulikana kama Panthou.

Waziri wa habari, Barnaba Marial Benjamin alisema kuondolewa wanajeshi hao kutaanza mara moja na shughuli hiyo itakamilika katika muda wa siku tatu.
Lakini katika habari inayotatanisha kutoka Khartoum inasema majeshi ya Sudan yamechukua eneo hilo, na si kweli kwamba Kusini inajitoa.

Sudan Kusini imekuwa chini ya shinikizo la kimataifa linalowataka kuondoka Heglich, ambayo ilikuwa chini ya udhibiti wa Sudan hadi April 10. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon alirudia shinikizo hilo la kuwataka Sudan Kusini waondoke katika eneo siku ya Alhamis.

“Ninawataka Sudan Kusini iondoe haraka majeshi yake kutoka Heglig. Huu ni uingiliaji wa uhuru wa Sudan na ni kitendo kinachoelezea wazi ukiukaji wa sheria.”

Benjamin alisema Kusini inatambua Heglig kuwa sehemu ya eneo lake na inataka mamlaka katika eneo hilo na maeneo mengine kutambuliwa na usuluhishi wa kimataifa.

Wiki hii, Rais wa Sudan Omar al-Bashir alitishia kuingia katika vita na Sudan Kusini na kuifundisha somo serikali ya Kusini kwa lazima.

Pande hizo mbili za Sudan na Sudan Kusini hazijaweza kutatua mizozo inayowakabili juu ya mipaka, mafuta na suala la uraia tangu Kusini ilipotangaza uhuru wake , mwezi Julai mwaka jana.

Kabla ya kujitenga kwao kaskazini na Kusini walipigana vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka 21 ambavyo vilipelekea Kusini kujitenga na kuwa huru.

XS
SM
MD
LG