Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 15:21

Tuhuma za rushwa ANC

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma.
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma.

Chama tawala nchini Afrika Kusini African National Congress kinachukua hatua za kinidhamu kwa mmoja wa wanachama wake ambaye ni kiongozi wa juu wa chama cha wafanyakazi nchini humo ambaye amekuwa akizungumzia waziwazi kuwepo kwa rushwa katika chama hicho.

Zwelinzima Vavi, ambaye anaongoza tawi la chama cha wafanyakazi nchini humo aliwakasirisha wakuu wa chama cha ANC alhamisi iliyopita pale alipowatuhumu rais Jacob Zuma kwa kutochunguza tuhuma za kuwepo kwa rushwa dhidi ya mawaziri waandamizi.

Wanachama wa chama cha ANC wameripotiwa kuwa wameamua katika mkutano wao wa jana kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya Vavi, lakini haijaelezwa ni hatua gani itachukuliwa dhidi yake.

XS
SM
MD
LG