Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:37

Somaliland yataka kutambuliwa kimataifa kama nchi


Waziri wa mambo ya nje wa Somaliland, Sa'ad Ali Shire.
Waziri wa mambo ya nje wa Somaliland, Sa'ad Ali Shire.

Zaidi ya raia milioni moja wametia sahihi wakitoa wito wa kutambuliwa Somaliland na jumuiya ya kimataifa, Rais wa Somaliland Ahmed Mohamed Silanyo aliwaambia waandishi wa habari Jumanne huko Hargeisa.

Somaliland ilijitenga kutoka Somalia mwaka 1991 baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka mitatu. Eneo hilo tangu wakati huo linajiendesha kwa mamlaka yake yenyewe, lakini hakuna taifa lolote limetambua uhuru wake.

Katika kujibu ombi hilo Somalia imerudia tena wito wa kutaka kuungana. Maafisa wa Somaliland walisema wamekusanya sahihi kutoka kwa nwatu milioni moja kutoka maeneo sita ya Somaliland tangu mwezi April.

Mandhari ya mji wa Hargeisa huko Somaliland. Machi 29, 2016.
Mandhari ya mji wa Hargeisa huko Somaliland. Machi 29, 2016.

Waziri wa mambo ya nje wa Somaliland, Sa’ad Ali Shire aliiambia sauti ya Amerika kwamba mtu atasoma taarifa inayotoa wito wa kutambuliwa Somaliland. Kama hawawezi kusoma mtu mwingine atawasomea. Somaliland ina sarafu yake yenyewe, jeshi na katiba iliyopigiwa kura kufuatia kura ya maoni mwaka 2001.

Bwana Shire alisema sahihi hizo zitapelekwa kwa viongozi wa kimataifa wakiwemo Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika. Serikali ya Somalia wakati wote inasisitiza Somaliland ni sehemu ya Somalia.

XS
SM
MD
LG