Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:26

Wanane wauawa katika mapigano Somalia


Mapigano kati ya makundi ya upinzani ya ki-Islam katika mji mkuu wa Somalia yameuwa watu wasiopungua wanane.

Mapigano kati ya makundi ya upinzani ya ki-Islam katika mji mkuu wa Somalia yameuwa watu wasiopungua wanane.

Mashahidi wanasema wapiganaji kutoka kundi la al-Shabab na Hizbul Islam walipigana Jumatatu jioni huko kusini mwa Mogadishu jirani na Labadhagah.

Shirika la habari la Ufaransa linaripoti kuwa wapiganaji sita wa Hizbul Islam walifyatuliwa risasi na kuuwawa na watu wenye silaha waliokuwa ndani ya basi dogo. Ripoti zinasema wapiganaji wawili wa al-Shabab waliuwawa dakika chache baadaye nje ya msikiti mmoja katika kulipiza kisasi.

Makundi hayo mawili yanapigana na serikali ya muda ya Somalia na kati yao wanadhibiti eneo kubwa la Mogadishu na kusini mwa Somalia. Makundi hayo yamekuwa washirika kwa muda mrefu, lakini pia yamekuwa yakipigana juu ya mamlaka na masuala mengine.

Jumatatu Rais wa Somalia Sheikh Sharif Sheikh Ahmed aliomba msaada wa dharura wa kijeshi kwenye mkutano wa viongozi wa Jumuia ya Ushirikiano wa Maendeleo katika nchi za Afrika mashariki-IGAD.

Viongozi wa nchi kadhaa waliohudhuria mkutano wa IGAD waliahidi kupeleka haraka wanajeshi 2,000. Wanajeshi hao wataongeza nguvu ya wanajeshi waliopo kutoka Umoja wa Afrika kusaidia kuilinda serikali ya Somalia. Jeshi la Umoja wa Afrika limesaidia kudhibiti maeneo muhimu nchini Somalia ikiwemo uwanja wa ndege, bandari na makazi ya Rais. Somalia haijawahi kuwa na serikali kuu thabiti tangu mwaka 1991.

XS
SM
MD
LG