Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 27, 2023 Local time: 04:46

UN yataka Somalia kulinda waandishi


Watangazaji katika radio Qaran mjini Mogadishu, June 28, 2013.

Umoja wa Mataifa umeitaka Somalia kufanya juhudi zaidi kulinda uhuru wa vyombo vya habari na kujieleza nchini humo ambamo waandishi wa habari 30 wameuawa katika kipindi cha miaka minne iliyopita.

Lakini Umoja wa Mataifa umesema pia katika ripoti yake mpya kwamba kumekuwa na maendeleo katika juhudi za kulinda waandishi wa habari Somalia katika miaka ya hivi karibuni.

Ripoti hiyo iliyotayarishwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa Somalia inatoa mfano wa kupitishwa kwa sheria ya vyombo vya habari Januari mwaka huu ambao “una hakikisha haki kadha, ikiwa ni pamoja na haki ya kutoa habari.”

Hatari dhidi ya waandishi wa habari na wafanyakazi wa umma ilidhihirika zaidi nchini Somalia kati ya august 2012 na juni 2016 ambapo waandishi 30 na wabunge 18 waliouawa nchini humo.

XS
SM
MD
LG