Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 02:33

Somalia na UAE wameanza mazungumzo ya kidiplomasia


Waziri wa mambo ya nje wa Somalia, Ahmed Isse Awad
Waziri wa mambo ya nje wa Somalia, Ahmed Isse Awad

Serikali ya Somalia ilisema Jumatatu kwamba imeanza mazungumzo ya maridhiano na viongozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu-UAE siku moja baada ya UAE kusema itasitisha program ya mafunzo kwa jeshi la Somalia katika taifa hilo la Afrika mashariki.

Mazungumzo yanalenga kusuluhisha ugomvi wa kidiplomasia baada ya jeshi la usalama la Somalia kukamata mabegi matatu ya fedha taslim kutoka katika ndege moja ya kiraia iliyosajiliwa UAE kwenye uwanja wa ndege wa Mogadishu April 8. UAE ilisema fedha hizo dola milioni 9.6 zilikuwa na lengo la kuwalipa mishahara wanajeshi 2,407 wa Somalia na kuendesha vituo vitatu vya mafunzo.

Ndege iliyobeba mabegi ya fedha taslim ambayo ilizuiwa Somalia
Ndege iliyobeba mabegi ya fedha taslim ambayo ilizuiwa Somalia

UAE haikuvitaja vituo hivyo vitatu vinavyoaminika kuwa mjini Mogadishu, Bosaso na Kismayo, mahala ambako kituo kipya kilichojengwa bado hakijazinduliwa rasmi.

Serikali ya Somalia ilisema fedha hizo zinashikiliwa na benki kuu na inasubiriwa uchunguzi kuona kama kweli zilikuwa za kuwalipa mishahara wanajeshi au kuwahonga wanasiasa ili kusababisha ukosefu wa uthabiti katika nchi. Waziri wa mambo ya nje wa Somalia, Ahmed Isse Awad aliiambia Sauti ya Amerika-VOA kwamba mazungumzo yameanza kati ya uongozi wa juu kutoka nchi hizo mbili na yanaendelea vizuri. Hakuelezea ni mahala gani au mfumo wake, lakini alisema hakuna nchi ya tatu inayosimamia mazungumzo hayo.

XS
SM
MD
LG