Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 13:20

Waziri Mkuu wa Somalia akataa kujiuzulu


Wakazi wa Mogadishu wakiandamana kumuunga mkono Waziri Mkuu wa Somalia, Mohamed Abdullahi Mohamed, kukaidi mpango wa kujiuzulu
Wakazi wa Mogadishu wakiandamana kumuunga mkono Waziri Mkuu wa Somalia, Mohamed Abdullahi Mohamed, kukaidi mpango wa kujiuzulu

Waziri Mkuu wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed anakataa kujiuzulu, na kukaidi mpango uliopendekezwa na Rais na spika wa bunge ilikuwezesha kuundwa kwa serikali mpya.

Waziri Mkuu Abdullahi Mohamed alisema Jumanne kwamba ataendelea kubaki madarakani kufuatia uungaji mkono kutoka kwa wananchi ikiwa ni pamoja na maandamano yaliyofanyika mjini Mogadishu.

Bwana Mohamed alisema atajiuzulu, iwapo tu bunge litamfuta kazi. Wiki iliyopita, Rais wa Somalia Sheikh Sharif Sheikh Ahmed na spika wa bunge Sharif Hassan Sheikh Aden, walitia saini mkataba uliokuwa na lengo la kuepusha mgogoro wa kisiasa mjini Kampala.

Mamlaka ya serikali ya mpito nchini Somalia inamalizika mwezi Agasti na viongozi wa Somalia wana hitilafiana juu ya namna ya kuendelea baada ya hapo.

Mkataba uliakhirisha uchaguzi wa rais hadi mwezi Agasti mwaka 2012, lakini pia ulisema Waziri Mkuu Mohamed, lazima ajiuzulu katika muda wa siku 30, na nafasi yake kuchukuliwa na Waziri Mkuu mpya ambaye atateuwa baraza jipya la mawaziri.
Somalia haija
wa na serikali kuu thabiti katika muda wa miaka 20, tangu wababe wa vita walipompindua diktekta Mohamed Siad Barre.

Mapigano yasiyoisha ya ndani kwa ndani yamezuiya kuwepo na mafanikio katika serikali kutokana na nchi hiyo kuwa na matatizo ya kudumu. Serikali iliyoko sasa inajaribu kuchukua tena udhibiti wa sehemu ya mji mkuu na kusini mwa Somali, maeneo yanayoshikiliwa na kundi la waasi la wanamgambo wa ki-Islam la al-Shabab.

XS
SM
MD
LG