Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 21, 2024 Local time: 07:48

Watatu wafariki dunia katika mlipuko wa bomu Mogadishu


Askari akitazama gari baada ya mlipuko mjini Mogadishu, Somalia, June 26, 2016.
Askari akitazama gari baada ya mlipuko mjini Mogadishu, Somalia, June 26, 2016.

Maafisa wa usalama ma mashahidi wanasema mlipuko wa bomu lililotegwa ndani ya gari umetokea nje ya gereji ya kutengeneza matairi katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu jioni ya Jumpili na kusababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi wanne wengine.

Mwandishi wa voa anasema dereva anayeshukiwa ni mjitoamuhanga kulipua bomu wa kundi la Al-Shabab ni miongoni mwa waliofariki.

Mwandishi wa habari wa kituo cha redio cha Dalsan mjini Mogadishu ambacho kipo karibu na eneo la mlipuko huo anasema alisikia mlipuko mkubwa na baadaye kuona moshi ukifuka na moto.

Mwandishi huyo anasema polisi wanafanya uchunguzi ili kuweza kufahamu shabaha ya shambulizi hilo.

Mohamed Abdulle afisa wa Polisi ambaye alikuwa mmoja wa waliokwenda kutoa huduma aliiambia VOA kwamba mmoja wa wafanyakazi wa gereji hiyo na mpita njia ni miongoni mwa watu waliouwawa.

XS
SM
MD
LG