Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 00:45

Mashambulizi ya helikopta Somalia


Mashahidi huko Somalia wanasema helikopta moja iliyokuwa na silaha imeshambulia jengo moja katika mji uliodhibitiwa na al-Shabab.

Mashahidi huko Somalia wanasema helikopta moja iliyokuwa na silaha imeshambulia jengo moja katika mji uliodhibitiwa na kundi la wanamgambo wa al-Shabab.

Wakazi wa Marka, kusini ya Mogadishu wanasema helikopta hiyo ilifyatua risasi kwenye nyumba iliyoshukiwa kuwa makamanda wa al-Shabab hukutana. Wanasema helikopta hiyo iliondoka baada ya majeshi ya wanamgambo wa ki-Islam kuwajibu kwa kuifyatuliaa risasi.

Mashahidi wanasema wanahisi helikopta hiyo ilitokea kwenye meli moja katika mwambao wa pwani. Hakuna ripoti za vifo wala kundi lolote kudai kuhusika na shambulizi hilo

Kamanda wa kundi la al-Shabab, Salah Ali Salah Nabhani aliuawa katika shambulizi la helikopta ya Marekani katika mji wa Barawe mwaka jana. Majeshi ya wanamaji ya Marekani kwa ushirikiano na majeshi ya nchi zingine yanafanya doria kupambana na maharamia katika pwani ya Somalia.

Kundi la wanamgambo wa al-Shabab linadhibiti maeneo ya kusini na katikati ya Somalia yakiwemo baadhi ya maeneo ya mji mkuu Mogadishu. Kundi hilo linajaribu kuiangusha serikali ya mpito ya Somalia na kuifanya Somalia kuwa chini ya sheria kali za kiislam.

XS
SM
MD
LG