Hayo yakiendelea muda wa mwisho wa wanajeshi waliosalia wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika kuondoka ukikaribia Desemba.
Rais Mohamud, akiwa anahudumu muhula wake wa pili, amesema mwezi Agosti alitaka kukimaliza kundi hilo mapema mwaka ujao.
Muda wa mwisho ni Desemba 2024 wakati kikosi cha ATMIS kinapaswa kuondoka nchini humo, rais Mohamud aliwambia wajumbe kwenye mkutano ulofanyika katika taasisi ya Royal United Services ya London.
Lengo lilikuwa kumaliza wapiganaji walobaki wa al Shabaab, aliongeza kusema.
Kazi hiyo ilifanywa kuwa ngumu zaidi na mafuriko mabaya ya hivi karibuni, ingawa pia yamefanya kuwa vigumu kwa wanamgambo hao kuendeleza mashambulizi ya mabomu ya ardhini, alisema.
Forum