Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 24, 2024 Local time: 20:32

AMISOM wazuia shambulizi la al-Shabaab

Mwanajeshi wa kisomali akilinda kwenye eneo karibu la sehemu ambako wanamgambo wa al-Shabaab walifanya shambulizi kwenye kituo cha jeshi.
Mwanajeshi wa kisomali akilinda kwenye eneo karibu la sehemu ambako wanamgambo wa al-Shabaab walifanya shambulizi kwenye kituo cha jeshi.

Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) inasema vikosi vyake pamoja na vile vya serikali ya Somalia vimezuia shambulizi lililopangwa kutekelezwa na wanamgambo wa al-Shabab.

Ripoti iliotolewa mapema leo imesema kuwa wanamgambo hao walijaribu kushambulia vikosi hivyo pamoja na majengo ya serikali kwenye mji wa Janale ulioko katika eneo la Lower Shabelle. AMISOM wanasema kuwa al-Shabab wamepata maafa makubwa bila kutoa taarifa yoyote ya iwapo kulikuwa na majeraha upande wa AMISOM.

XS
SM
MD
LG