Somalia imesema imemfukuza balozi wa Ethiopia mjini Mogadishu na kuamuru kufungwa kwa balozi ndogo mbili ambapo moja katika mkoa wa Puntland wenye utawala kiasi na katika jamhuri iliyojitenga ya Somaliland katika mzozo kuhusu makubaliano ya bandari.
“uingiliaji kati wa wazi wa serikali ya Ethiopia katika masuala ya ndani ya Somalia ni ukiukaji wa uhuru na utaifa wa Somalia,” imesema ofisi ya Waziri Mkuu katika taarifa yake ya leo alhamisi.
Uamuzi huo unafuatia mkutano wa baraza la mawaziri uliokuwa chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu Hamza Barre mjini Mogadishu. Taarifa tofauti iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje imesema ilimuamuru blaozi wa Ethiopia Mukhtari Mohamed Ware kuondoka nchini ndani ya saa 72 kuanzia leo Alhamisi.
Forum