Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 14, 2024 Local time: 00:08

Ndege zashambulia al-Shabab Somalia


Pwani ya Somalia
Pwani ya Somalia

Wanamgambo wasiopungua wanane wa al-Shabab inashukiwa wameuawa katika shambulizi ya ndege aina ya Drone karibu na kijiji cha Baladul Amin, kiasi cha kilomita 120 kaskazini-magharibi ya Mogadishu.

Wakazi wa eneo hilo wameiambia Sauti ya Amerika kuwa makamanda wapatao watatu wa ngazi za chini ni miongoni mwa waliouawa.

Wenyeji wanasema walisikia milipuko mitatu mikubwa mashambulizi hayo ya anga yalipopiga katika maeneo ya al-Shabab mapema Jumapili.

Wenyeji pia wanasema wanaamini mashambulizi hayo yalifanywa na ndege za Marekani za Drone lakini wizara ya ulinzi ya marekani – Pentagon – haijathibitisha habari hiyo.

Marekani imekuwa ikitumia mashambulizi ya drone dhidi ya viongozi wa al-Shabab, ikiwa ni pamoja na lile dhidi ya kiongozi wa kundi hilo, Ahmed Abdi Godane, ambaye aliuawa katika shambulizi la drone Septemba 2014.

XS
SM
MD
LG