Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 17:11

Somalia: Al Shabab washambulia kambi inayolindwa na wanajeshi wa Uganda


Ramani ya Somalia
Ramani ya Somalia

Maafisa nchini Somalia wanasema wanamgambo wa Al-Shabab mapema Ijumaa walishambulia kambi ya kijeshi inayolindwa na wanajeshi wa Uganda wa kikosi cha Umoja wa Afrika, vyanzo kadhaa vimesema.

Shambulio la alfajiri lilifanyika huko Bulo Marer, mji wa kilimo katika jimbo la Lower Shabelle, umbali wa kilomita 110 kusini mwa Mogadishu.

Wanamgambo hao walililipua mabomu manne hadi sita, yakiwemo mabomu yaliyotegwa ndani ya magari yaliyokuwa yakiendeshwa na washambuliaji wa kujitoa muhanga, vyanzo vitatu ambavyo vimeomba majina yao yahifadhiwe vimeiambia idhaa ya Kisomali ya Sauti ya Amerika.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, wanamgambo hao walijipenyeza karibu na kambi hiyo baada ya milipuko hiyo, iliyofuatiwa na mapigano makali ya risasi.

Wanamgambo hao walionekana ndani ya mji wa Bulo Marer. Kambi iliyoshambuliwa iko nje kidogo ya mji huo.

Kundi la Al Shabab mapema Ijumaa lilituma ujumbe kupitia mtandao wa Telegram likidai kuwa lilishambulia vikali kambi hiyo. Uongozi wa jeshi la Umoja wa Afrika na serikali ya Somalia walikuwa hawajatoa maelezo juu ya shambulio hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG