Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 11:07

Hanafi vipi aliacha uandishi na kuwa muuaji wa Al-Shabab


Hassan Hanafi Haji
Hassan Hanafi Haji

Mwandishi wa habari wa zamani wa Somalia, Hassan Hanafi Haji alinyongwa mjini Mogadishu Jumatatu kwa kuhusika kwake katika mauaji ya waandishi wenzake watano kama sehemu ya kampeni ya kundi la kigaidi la Al Shabaab kudhibiti vyombo vya habari vya ndani.

Moja ya malengo ya kwanza ya Hanafi ilikuwa ni kituo maarufu binafsi cha radio cha Horn Afrik.

"Alikuwa ni hatari miongoni mwetu,: anasema mwandishi mwenzake Falastin Iman, ambaye aliamka akisikia milio ya risasi siku moja asubuhi ya mwezi Agosti mwaka 2007 na kubaini kuwa mwenzake wa Radio Afrika, Mahad Mohamed Elmi amepigw risasi nje ya mlango wake.

Pale walipoufikisha mwili wa Elmi hospitali, Hanafi alikuwa akisubiri.

Iman anasema alikuwa hapo kutaka kufahamu hali ya Mahad, kama amefariki au bado alikuwa hai. "Alikuwa mtu hatari sana kwa waandishi wa habari kwasababu alitufahamu sote. Hakuwa sawa na wanachama wengine wa Al Shabaab," ameongezea.

Hanafi alihudhuria mazishi ya Elmi. Katika ushuhuda wake ulioonyeshwa kwenye televisheni ambao aliutoa alisema ulipatikana baada ya kuteswa. Hanafi amesema alihudhuria mazishi kuitambua gari iliyotumiwa na Imam na mkurugenzi wa Radio Afrik, Ali Iman Sharmarke.

Wakiondoka kwenye shughuli hiyo, gari yao ilipigwa na bomu la kutegwa kando ya barabara. Sharmarke aliuawa. Imam alijeruhiwa kichwani na chuma.

"Wakuu wangu hawakuwa wakifurahishwa na mwandishi huyo, walikuwa wakiniita na kuniula kuhusu mwandishi fulani," Hanafi ameiambia televisheni ya taifa ya Somalia. "Nilikuwa nawapati habari. Mara nyingine wananijulisha mwandishi anayelengwa na mara nyingine hawanielezi kitu."

Kufuatilia habari za Hanafi kuanzia alivyokuwa mwandishi wa radio mpaka kuwa wakala wa Al Shabaab, VOA imezungumza na waandishi wenzake wa zamani, akiwemo Liban Abdi Ali, ambaye alifanya kazi na Hanafi kwenye Radio Voice of Quran.

"Nilimfahamu kama mtu ambaye anapenda kuwa na wakati mzuri na marafiki zake," Ali anakumbuka hilo. Mabadiliko yalianza, anasema wakati Hanafi alipoanza kuripoti habari kutoka kwenye mahakama za kiislamu, hapo akawa mtu tofauti, mpenda ghasia, aliyejaa chuki na mwenye kutoa taarifa za kukashifu waandishi wenzake, hasa marafiki zake wa zamani ameongezea.

Ali anasema baadhi ya wenzake walijaribu kumuondoa katika mwelekeo huo, lakini alikuwa mwenye msimamo mkali na hata kiitikadi na kuwa tayari kufa.

Mwandishi wa habari Abdirahman Yusuf Al-Adala alikuwa akikaa pamoja na Hanafi, alipoanza kuwa ni mtu wa msimamo mkali, Al-Adala anasema Hanafi "siku zote alikuwa akiniita ama kunitishia au kuniambia kuhusu jinsi mwandishi fulani alivyouawa lengo likiwa kunitisha kwa maneno makali juu ya vifo vya wenzangu."

hanafi alipowakaribisha waandishi wa habari Febriaru 2009 kwenye mkutano wa waandishi, wanachama wa Al-Shabaab waliokuwa na silaha walimuua mkurugenzi wa Horn Afrika Sa'id Tahlil Ahmed.

"Tulimuona akifa mbele ya macho yetu, Al-Adala anasema. "Hanafi alifahamu kuhusu kuuliwa na alifanikisha hilo. Siku hiyondiyo nikabaini kuwa mwenzangu huyo alikuwa mtu katili sana."

Hata baada ya Al-Adala kujiunga na radio ya taifa Radio Mogadishu kwasababu ilikuwa ikilindwa na walinzi wa amani wa Umoja wa Afrika, anasema Hanafi "siku zote alikuwa akiinipigia dakika chache baada ya mwandishi kuuawa mjini Mogadishu, kijeuri akisema fulani ameonja adhabu ya Mujahidin."

Al-Adala ambaye hivi sasa ni mkurugenzi wa shirika la habari la serikali anasema Hanafi alikuwa tishio kubwa kwa maisha yake bila ya yeye kufahamu hilo.

Ahmed Abdirahman Jaakat aliingia kuongoza vipindi katika Horn Afrika baada ya vifo vya wakurugenzi wawili wa awali wa kituo hicho. Anasema Hanafi aliamuru aicheze kanda ya kaseti ya Al-Shabaab. Alipokataa kufanya hivyo, vikaanza vitisho vya kuuliwa ambavyo alivipokea kwenye simu yake ya mkononi.

Viisho vilisema, kama usipoacha unachofanya, utawafuata marafiki zao, hiyo ikimaanisha kuwa waandishi wenzangu ambao waliuawa, anasema Jakaat ambaye alikimbia Mogadishu na kwenda katika jimbo la Minnesota hapa Marekani.

Kampeni za Al-Shabaab kuvinyanyasa vyombo vya habari kulipelekea waandishi wa habari wa Somalia kujidhibiti wenyewe, hasa pale inapokuja kuripoti mashambulizi yaliyokuwa yakifanywa na kundi hilo, anasema mchambuzi wa siasa Abdiwahab Sheikh Abdisamad akiwa mjini Nairobi.

anasema kuwalenga waandishi wa habari kulimaanisha kuitisha jamii ya kisomali kwa kuimarisha umuhimu wa ujumbe wa Al-Shabaab, ambapo Abdisamad anasema ni pamoja na kujigamba, "tunaweza kuja hapo ulipo. Tunaweza kumlenga mtu yoyote mjini humo na tunaweza kusababisha vifo kwa jamii."

Kwa Falastin Iman, ujumbe ulikuwa wa pande mbili. "Mimi ni mwandishi mwanamke, kwahiyo vitisho kwangu vilikuwa mara mbili," anasema.

Iman, ambaye hivi sasa ni mwandishi wa VOA katika idhaa ya Kisomali anasema Hanafi na Al-Shabaab walifanya kazi "kuwanyanyasa waandishi ili kuwaonyesha waandishi wengine kwamba, tutawafanyia hivyo hivyo kama tulivyofanya kwa kundi hili, kwahiyo lazima ufuate amri zetu. Walikuwa wanataka kudhibiti matukio ya habari ya kila siku katika ofisi zetu, habari zetu, vipindi vyetu."

Bada ya kukamatwa nchini Kenya mwaka 2014, hanafi alikuwa mmoja wa washukiwa wachache wa Al-Shabaab kukabiliwa na mashtaka kwenye serikali ya Somalia kufuatia miaka kadhaa ya ukosoaji wa makundi ya haki za binadamu kwamba mamlaka inahitaji kufanya mengi zaidi.

Kamati ya kulinda waandishi inasema Somalia ni moja ya nchi hatari sana duniani kwa wandishi wa habari.

Kunyongwa kwa Hanafi kumekuja siku chache baada ya wanamgambo wengine wawili wa Al-Shabaab kunyongwa kwa kumuua mwandishi kwa bomu la kwenye gari mwaka jana. Mwandishi huyo alikuwa mjane wa mwandishi mwingine ambaye aliuawa mjini Mogadishu mwaka 2012.

XS
SM
MD
LG