Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 08:45

Somali na Somaliland wamaliza mkutano wao London


Washiriki katika mkutano wa Somalia na Somaliland mjini London
Washiriki katika mkutano wa Somalia na Somaliland mjini London

Somalia inakumbana na kazi kubwa ya kuunda serikali thabiti huku ikipambana na na wanamgambo wa kundi la al-Shabab wanaotaka nchi hiyo kuwa taifa la kiislam

Siku mbili za mazungumzo ya kwanza kabisa kuwahi kufanyika kati ya Somalia na mkoa uliojitenga wa Somaliland yamemalizika karibu na London siku ya Alhamis. Pande zote zimekubaliana kwamba lazima mazungumzo yaendelea.

Waziri wa mambo ya ndani wa Somalia Abdisamad Moalim Mohamud aliiambia Sauti ya Amerika, Idhaa ya Kisomali kwamba pande zote mbili zilikubaliana kushirikiana katika mapambano dhidi ya ugaidi, uharamia, uvuvi haramu na kutupa taka za sumu. Amesema pia wamekubaliana kuepuka jambo lolote ambalo litadumaza mazungumzo.

Katika matamshi yake kwa VOA waziri wa mambo ya nchi za nje wa Somaliland, Mohamed Abdillahi Omar, alisema siku mbili za mazungumzo zilikuwa na mafanikio. Alisema walibuni mpango wa mazungumzo wa baadae juu ya masuala ambayo yanausiana na pande zote.

Uingereza na Umoja wa Ulaya walipanga mkutano kama sehemu ya juhudi zao za kuisaidia Somalia kupambana na ugaidi. Somalia inakumbana na kazi kubwa ya kuunda serikali thabiti huku ikipambana na juhudi za kutokomeza wanamgambo wa al-Shabab wanaotaka kuigeuza Somalia kuwa taifa la kislamu la kihafidhina .

Somaliland ilijitenga kutoka Somalia wakati serikali ya Somalia ilipopinduliwa mwaka 1991. Lakini hakuna nchi yeyote au kiongozi yeyote wa dunia anayetambua uhuru wa Somaliland.
XS
SM
MD
LG