Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 09:50

Idadi ya vifo yaongezeka Mogadishu


Eneo lililoshambuliwa kwa mabomu Mogadishu, Somalia Jumatatu.
Eneo lililoshambuliwa kwa mabomu Mogadishu, Somalia Jumatatu.

Idadi ya vifo kutokana na mashambulizi mawili ya bomu mjini Mogadishu Jumatatu imeongezeka na kufikia tisa.

Idadi ya vifo kutokana na mashambulizi mawili ya kwenye gari ya kujitoa muhanga ya Jumatatu karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mogadishu imefikia 9 baada ya waokozi kugundua miili ya watu wawili Jumanne kwenye vifusi vya jengo la hoteli ya Peace iliolengwa na mmoja wa washambuliaji.

Maafisa wa eneeo wameiambia VOA idhaa ya Kisomali Jumanne kwamba miili ya mwanake na mwanaume ilionekana kwenye ukuta kupitia kamera za usalama za hoteli hiyo. Takriban watu 21 walijeruhiwa kwenye mashambulizi hayo ambayo kundi la kigaidi la al Shaabab limedai kuhusika.

Hii ni mara ya pili kundi hilo kufanya mashambulizi yanayofatana la kwanza likilenga kuleta hali ya taharuki kisha la pili likilenga kufanya uharibifu mkubwa.

XS
SM
MD
LG