Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 29, 2023 Local time: 02:06

Waasi waua 3 Somalia mwanzo wa Ramadhan


Wapiganaji wa al-Shabaab katika mafunzo
Wapiganaji wa al-Shabaab katika mafunzo

Kundi la waasi la al-Shabab limeuwa wanajeshi watatu wa vikosi vya usalama Somalia katika mji mkuu Mogadishu Jumapili katika siku ya kwanza ya mwezi wa Ramadhan nchini humo. Polisi wanasema kundi hilo lilisema kuwa litafanya mashambulizi wakati wa mwezi wa Ramadhan.

Walinzi wa amani wa serikali na Umoja wa Afrika wameongeza doria za ulinzi kujaribu kuzuia mashambulizi wakati kutoka kundi hilo ambalo limekuwa likipigana na serikali kwa miaka saba sasa likidai kutaka kuleta shara za kiislamu nchini humo.

Polisi wawili wa kuongoza magari barabarani walipigwa risas katika barabara moja maarufu mjini Mogadishi, Maka al-Mukaram, kulingana na maelezo ya kamanda wa polisi mjini humo, Ali Hirsi.

Katika eneo la kaskazini mwa mji huo, mwanajeshi mmoja alipigwa risasi na watu waliokuwa na bastola nje ya duka moja, kulingana na maelezo ya mwenye duka aliyeshuhudia mauaji hayo.

XS
SM
MD
LG