Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 16:20

Sokwe mkongwe Uganda afariki


Familia ya masokwe porini
Familia ya masokwe porini

Sanamu ya sokwe huyo itajengwa mahali alipozikwa kuwa ukumbusho wa mchango wake katika kuleta watalii Uganda

Ruhondeza alikuwa baba wa familia ya sokwe iitwayo Mubare ambayo imekuwa ikuwavutia watalii kuanzia miaka ya tisini. Lakini kwa nini akaitwa Ruhondeza? msemaji wa shirika la wanyama pori nchini Uganda Lilian Nsubuga jina la sokwe huyo liliashiria tabia yake. Alikuwa mzembe sana na alipenda kulala sana. Ruhondeza ni jina ambalo linamaanisha mtu anayependa kulala na linatokana na lugha ya kabila la Bafumbira nchini Uganda.

Ingawa Ruhondeza alikuwa na tabia ya kuzembea zembea na kujivuta vuta, upande wa wanawake hakuzembea hata kidogo. Bi BNsubuga anasema aliwakasirikia sana wanaume wa familia yake walipojaribu kuwatongoza wanawake wake. Alikuwa mkali sana kiasi kwamba kwa wakati mmoja hakuwa na mrithi kwa sababu wanaume wengi wa familia yake walitoroka kuukwepa ukali wake. Kwenye ulimwengu wa sokwe, wanawake wote ni wa sokwe anayeiongoza familia.

Siku za mwisho za Ruhondeza zilijaa upweke. Ingawa haijulikani aliwazaa watoto wangapi, kinachojulikana ni kwamba aliwazaa watoto wengi lakini wakati wa kufa kwake alikuwa peke yake.

Mwanzoni mwa mwaka huu, familia ya sokwe mwengine aitwaye Mubare ilivaamia na sokwe wengine wa msituni na kwenye harakati za kupigana, baadhi ya sokwe walitoroka kuyanusuru maisha yao. Kijana mmoja wa Ruhondeza aitwaye Kanyonyi aliweza kuwaokoa jamaa saba wa familia yao na kutoroka nao. Wale wengine hawajulikani walipo. Baada ya vita hivyo Ruhondeza alijipata akiwa peke yake na hakuungana tena na familia yake.

Madaktari wa wanyama pori wanaufanyia uchunguzi mwili wa Ruhondeza ili kuthibitisha kilichokisababisha kifo chake. Ripoti ya kwanza ambayo imetolewa sasa inasema kifo chake kilisababishwa na uzee.

Maiti yake haikuwa na majeraha yoyote na meno yake yalikuwa yameharibika kabisa na wakati wa kifo chake hakuweza kula vizuri. Mwili wake ulikuwa umedhoofika kabisa na misuli yake kulegea legea. Ruhondeza alizikwa Juni 27. Sanamu ya ukumbusho itajengwa mahali alipozikwa Ruhondeza ili iwe ukumbusho wa maisha yake na mchango wake wa kuanzisha utalii wa sokwe nchini Uganda.

XS
SM
MD
LG