Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 23:12

Slaa anadai kuwepo na wizi wa kura Tanzania


Mtumishi wa kituo cha kupiga kura cha Mzambarauni akitayarisha vifaa vya kupiga kura
Mtumishi wa kituo cha kupiga kura cha Mzambarauni akitayarisha vifaa vya kupiga kura

Mgombea kiti wa chama cha upinzani cha CHADEMA huko Tanzania Dk. Wilbrod Slaa ameitaka tume ya uchaguzi kuhesabu upya kura, akidai kwamba anaushahidi wa kuwepo na kasoro na kile anachoeleza kwamba "wamechakachua kura" yani wamebadilisha matokeo kwa wizi.

Hadi Jumatano jioni tume ya uchaguzi imekua ikitoa matokeo ya sehemu kadhaa ya uchaguzi na haikutoa matamshi yeyote kutokana na madai ya upinzani. Kuchelewa kutangazwa kwa matokeo hayo yamesababisha kuzuka kwa hali ya wasi wasi katika kila pembe ya nchi na watu kuanza kuuliza kwanini inachukua muda huu wote kutangaza matokeo hayo.

Hii ni mara ya kwanza kabisa kuwepo na mvutano mkubwa katika kutangaza matokeo ya uchaguzi wa rais huko Tanzania tangu kuanza mfumo wa vyama vingi mwaka 1995.

Akizungumza na Sauti ya Amerika Dk Slaa anasema, "nimesoma ripoti ya awali ya wafuatiliaji wa kimataifa na wamesema taratibu nyingi zimekiukwa, lakini sijui ni taratibu gani kwa sababu taarifa yao kina haijatoka, nimesoma tu kwenye magazeti".

Lakini anasema jambo muhimu la kufahamu ni kwamba wafuatiliaji wa kimataifa hawafanyi kazi ya kina kama wanavyofanya wao.Kwani anasema wanachukua matokeo ya kila kituo na kuhesabu upya na kulinganisha na matokeo ya tume ya taifa na wameshuhudia kasoro nyingi.

XS
SM
MD
LG