Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 19:13

Jeshi la Syria lasema sitisho la mapigano ni la muda


Wakazi wakitembea karibu na majengo yaliyoharibiwa katika eneo linaloshikiliwa na waasi huko Old Aleppo, Syria.
Wakazi wakitembea karibu na majengo yaliyoharibiwa katika eneo linaloshikiliwa na waasi huko Old Aleppo, Syria.

Wakati Marekani na Russia zikiendelea kutafuta sitisho la mapigano nchini Syria, hasa katika kuokoa mji wa Aleppo, jeshi la Syria chini ya uongozi wa Rais Bashar al Assad, limesema itakuwa ni hatua ya muda tu.

Waasi wa Syria wameilaumu Russia kwa kutumia silaha kwenye wiki mbili za mashambulizi. Wakati ikiwa dhahiri kuwa lengo la Assad ni kuchukua mji wa Aleppo, wachambuzi wa Russia wanasema lengo la Kremlin ni kutambulika kimataifa.

Waziri wa mambo ya nje wa Russia, Sergei Lavrov, Juma hili ametoa tamko la matumaini ya kupata sitisho la mapigano wakati akiwa na mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Syria, Staffan de Mistura, walipokutana Jumatatu mjini Geneva pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry.

XS
SM
MD
LG