Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 12:44

Sitisho la mapigano lapelekea utulivu katika vita DRC


Wapiganaji wa M23 katika mji wa Rutshuru
Wapiganaji wa M23 katika mji wa Rutshuru

Rais wa Drc Felix Tshisekedi alihudhuria Mkutano huko Luanda Jumatano , ambapo kulifikiwa makubaliano ya kusitisha mapigano na kuweka silaha chini katika eneo la mashariki mwa Drc lililoharibiwa na vita .

Utekelezaji ulianza Ijumaa jioni. Waasi wa M23 ambao wameteka maeneo mengi Drc katika wiki za karibuni walitakiwa kujiondoa katika maeneo wanayokalia, na endapo watashindwa basi jeshi la pamoja la Afrika mashariki litaingilia.

Wakaazi wa ndani wanaripoti kwamba hadi Jumapili mchana hakukuwa na ahadi zozote za waasi kuondoka.

Mapigano yalikuwa yameendelea hadi muda wa mwisho wa kusitisha mapigano kaskazini mwa mji mkuu wa jimbo la Goma lakini siku ya Jumapili pande zote mbili zilikuwa zikishikilia misimamo yao , wakaazi wameliambia AFP kwa njia ya simu. Jumamosi wanamgambo wa Maimai na Democratic Forces for liberation of Rwanda –FDLR walipigana na M23 kwa ajili ya kudhibiti eneo la kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa jimbo la Goma ambako hakuna jeshi la taifa.

Matokeo yake M23 walichukua mji wa Kisharo kilomita 30 kutoka mpaka wa Uganda , wakaazi wamesema. AFP haikuweza kuthibitisha madai hayo kutoka kwa wakaazi.

XS
SM
MD
LG