Chama cha kikonservative kimeshinda uchaguzi huo lakini hakina idadi ya kutosha ya wabunge, kumuondoa madarakani utawala wa kisoshalisti wa waziri mkuu Pedro Sanchez.
Chama hicho, kikiongozwa na mgombea wake mkuu Alberto Nunez Feijoo, kilipata idadi ndogo ya kura ikilinganishwa na matarajio kutokana na ukusanyaji wa maoni uliofanyikwa awali.
Alberto amehutubia wafuasi wake akisema kwamba dhamira ya chama hicho sasa ni kuepusha hali ya sintofahamu, na kwamba wahispania wameweka Imani yao kwa chama hicho na kwamba vyama vyote vya kisisasa vilivyo na waakilishi bungeni vinstahili kufanya mazungumzo.
Amesema kwamba kama kiongozi wa chama chenye idadi kubwa ya wabunge, ataanzisha mazungumzo hayo na kuongoza serikali.
Japo chama cha Kisoshaliti, chake waziri mkuu Pedro Sanchez, kimemaliza katika nafasi ya pili, kimefurahia matokeo hayo pamoja na vyama vingine shirika, kwa sababu muungano wao unaweza kuwa na idadi kubwa ya wabunge ikilinganishwa na vyama vya PP na vya mrengo wa kulia.
Muungano wa Sanchez una viti 172 ikilinganishwa na chama cha Alberto Feijoo, chenye wabunge 170.
Forum