Mazishi ya Waziri Mkuu wa zamani wa Singapore Lee Kuan Yew yamefanyika Jumapili huku waziri mkuu Lee Hsien Loong akimwelezea marehemu kama mtu aliyeishi na kuipenda nchi yake kwa dhati hadi kifo chake.
Akitoa wasifu wa marehemu katika chuo cha kitaifa cha Singapore, waziri Mkuu Lee Hsien alisema; “mwanga uliotuongoza miaka yote hii umefifia, tumepoteza mwanzilishi wa taifa letu.”
Mazishi ya Lee Kuan Yew yalihudhuriwa na wageni mashuhuri kutoka nchi mbalimbali akiwemo rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton, Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe, rais wa Korea Kusini Park Geun –Hye na Waziri Mkuu wa Australia Tony Abbot.
Waziri Mkuu huyo wa zamani aliyongoza Singapore kutoka mwaka wa1959 hadi 1990. Alifariki Jumatatu akiwa na umri wa miaka 91.