Mke wa Rais wa zamani wa Ivory Coast, Simone Gbagbo, amefikishwa mahakamani Jumanne.
Simone Gbagbo, ambaye pia anafahamika kwa jina la “Iron Lady,” anashutumiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu, wafungwa wa kivita, na raiya. Inadaiwa kuwa alihusika kwenye ghasia nchini humo baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 ambazo ziliua zaidi ya watu 3,000.
Awali alikuwa amehukumiwa miaka 20 gerezani kwa kushambulia mamlaka za Serekali. Mume wake, Rais wa zamani Laurent Gbagbo na waziri wake wa vijana wa zamani Charles Ble Goude, wanakabiliwa na mashitaka mbele ya mahakama ya kimataifa ya ICC, kwa shutuma za kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 zilizokuwa na lengo za kumeweka Rais huyo madarakani baada ya kushindwa kwenye uchaguzi na Rais wa sasa Alassane Ouattara.