Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 30, 2023 Local time: 22:46

Sikukuu ya Krismas: Shambulio la kujitoa muhanga laua sita DRC


Picha hii kutoka timu ya waandishi ya Jeshi la Uganda iliyopo nao katika operesheni Shujja inayoendelea DRC.

Watu wasiopungua sita wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mlipuko uliotokea Beni, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Shambulizi hilo limetokea baada ya mtu mmoja kuripotiwa kutegua bomu katika sherehe za Krismasi.

Chini ya udhibiti mkubwa wa serikali tangu mwezi Mei, Jimbo la Kivu Kaskazini limeendelea kuathirika na ukosefu wa usalama na mlipuko huo umeongeza idadi ya mashambulizi ya hivi karibuni yanayofanywa na vikundi mbalimbali vyenye silaha vinavyofanya shughuli zao katika eneo hilo.

Kati ya wengine 13 waliojeruhiwa na kulazwa hospitali mbalimbali ni manaibu meya wawili wa maeneo ya Mulekera na Ruwenzori.

Ramani ya DRC
Ramani ya DRC

Maafisa wa jeshi wamekuwa wakiendesha utawala wa maeneo mashariki mwa DRC tangu Mei katika juhudi za serikali ya Kinshasa kudhibiti hali ya ukosefu wa usalama.

Kwa mujibu wa msemaji wa gavana wa kijeshi wa Kivu Kaskazini, Jenerali Sylvain Ekenge, shambulizi hilo limetokea saa mbili usiku kwa saa za huko siku ya Jumamosi, katika mlango wa kuingilia baa iliyokuwa imejaa wateja huko Ishango.

Amesema mshambuliaji alitegua bomu katika mlango wa kuingilia baa hiyo baada ya “kuzuiliwa na walinzi kutoingia katika baa hiyo iliyokuwa imefurika watu,” kulingana na taarifa ya afisa mmoja wapo.

Tamko lililotolewa na Rais Felix Tshisekedi limeahidi kuwafuatilia wahalifu hao waliofanya shambulizi hilo, wakisema “uhalifu huu hauwezi kuachiwa uende bila ya kuadhibiwa na waliofanya uhalifu huu watatafutwa na kuangamizwa.”

“Mkuu wa nchi amelaani shambulizi hilo la kinyama. Amepeleka salamu za rambirambi kwa waliouawa na familia zao,” iliongeza taarifa hiyo Jumapili.

Hili ni shambulizi la tatu la bomu katika mji wa Beni tangu mwezi Juni. Shambulizi la kwanza lililenga parokia ya Kanisa Katoliki katika ujirani wa Bustili, na kujeruhi waumini wawili waliokuwa wakifanya ibada.

Shambulizi la pili lilitokea katika eneo la vinywaji, na kumuua mlipuaji bomu wa kujitoa mhanga.

Kwa mujibu wa msemaji wa gavana wa kijeshi, magaidi wa ADF (Allied Democratic Forces), ambao wanaendesha operesheni zao wakiwa wamekata tamaa, wameanzisha vikundi vidogovidogo katika mji wa Beni na maeneo yanayozunguka kwa ajili ya kuwashambulia raia wasiokuwa na hatia.

“Wakati huohuo, majeshi ya Congo na Uganda ambayo yamekuwa yakifanya operesheni ya pamoja dhidi ya ADF tangu Novemba wanasema wameongeza mashambulizi upande wa mashariki ya DRC.

Chanzo cha habari hii ni gazeti la The East African la Kenya

XS
SM
MD
LG